Search This Blog

SALA NDIYO NJIA YETU KUU YA KUZUNGUMZA NA KUMFIKIA MUNGU, NA NDIYO NGUVU PEKEE INAYOWEZA KUMWOKOA MWANADAMU HAPA DUNIANI

Yesu na Maria

Yesu na Maria

Saturday, February 7, 2015

SALA YA ASUBUHI


Ee baba yetu mungu mkuu,umenilinda usiku huu,nakushuru kwa moyo,ee baba mwana na roho, nilinde tena siku hii,niache dhambi nikutii,naomba sana baba we,baraka zako nipokee,bikira safi , ee maria,nisipotee nisimamie,mlinzi mkuu malaika we,kwa mungu niombee,nitake nitende meme tu,na mwisho nije kwako juu amina.
Nia njema kumheshimu mungu wangu,namtolea roho yangu,nifanye kazi nipumzike,amri zake tu nishike,wazo neno tendo lote,namtolea mungu pote,roho mwili chote changu,pendo na uzima wangu,mungu wangu nitampenda,wala dhambi statenda,jina lako nasifia,utalo hutimia,kwa utii navumilia,teso na matata pia,nipe bwana neema zako,niongezee sifa yako.amina