Search This Blog

SALA NDIYO NJIA YETU KUU YA KUZUNGUMZA NA KUMFIKIA MUNGU, NA NDIYO NGUVU PEKEE INAYOWEZA KUMWOKOA MWANADAMU HAPA DUNIANI

Yesu na Maria

Yesu na Maria

Rozali Takatifu

NAMNA YA KUSALI ROZARI YA BIKIRA MARIA


 

Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk) .
Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.

Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika:
  • Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..
 Au;
  • Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,… Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, ..
Au;
  • Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,….. Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……
  • Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
  • Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi.
  • Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha hapo juu. Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Maria…, 
  • Atukuzwe..,    
  • Ee Yesu wangu…
  • Tuwasifu milele...
kama muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi hayo). 
Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na Tendo husika



ROZARI YA MOYO MTAKATIFU WA YESU


Tumia tasbihi ya kawaida yenye chembe ndogo 53.
Kwenye Msalaba Sali:
  • Ee Yesu tupe moyo wako kama amana ya upendo wako na kimbilio letu, ili tupate pumziko salama wakati wa maisha yetu na faraja tamu saa ya kufa kwetu.
  •  Baba Yetu ……..
  • Salamu Maria ……. (mara tatu)
  • Nasadiki ………..
 Kwenye chembe kubwa Sali (Badala ya ‘Baba Yetu’):
  • Ninakuabudu, ninakutukuza na ninakupenda, Ee Moyo wa Yesu wangu mpenzi, uliopenywa na huzuni nyingi kwa ajili ya dhambi, ambazo zimekuwa zikitendwa hata leo, dhidi ya Sakramenti Takatifu sana ya Altare. Ninakutolea hapo kwa kuridhika, moyo wa Mama yako mpendevu, na mastahili ya watakatifu. Amina.
 Kwenye chembe ndogo sali (Badala ya ‘Salamu Maria’):
  • Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu, uwakao mapendo kwetu, washa nyoyo zetu kwa mapendo yako
 Kisha sema Litania ya Moyo Mtakatifu wa Yesu

P.S. Mwezi wa sita ni wa kuuheshimu Moyo Mtakatifu wa Yesu. Kwa kusali Rozari ya Moyo Mtakatifu wa Yesu kila siku, waumini hujipatia neema na rehema nyingi.


7 comments: