Search This Blog

SALA NDIYO NJIA YETU KUU YA KUZUNGUMZA NA KUMFIKIA MUNGU, NA NDIYO NGUVU PEKEE INAYOWEZA KUMWOKOA MWANADAMU HAPA DUNIANI

Yesu na Maria

Yesu na Maria

Matendo Ya Rozari Takatifu


MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)

Tendo la kwanza
Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. 
Tumwombe Mungu  atujalie unyenyekevu.

Tendo la pili
Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti.  
Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.

Tendo la tatu; 
Yesu anazaliwa Betlehemu.  
Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara

Tendo la nne
Yesu anatolewa hekaluni.  
Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.

Tendo la tano
Maria anamkuta Yesu hekaluni.  
Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.


MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)

Tendo la kwanza; 
Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.  
Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.

Tendo la pili; 
Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu.  
Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.

Tendo la tatu; 
Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. 
Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.

Tendo la nne
Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu.  
Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.

Tendo la tano;
Yesu anakufa Msalabani. 
Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.


MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)

Tendo la kwanza; 
Yesu anafufuka.  
Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.

Tendo la pili; 
Yesu anapaa mbinguni
Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.

Tendo la tatu; 
Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. 
Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.

Tendo la nne; 
Bikira Maria anapalizwa mbinguni. 
Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.

Tendo la tano
Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni.  
Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.



MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)

Tendo la kwanza; 
 Yesu anabatizwa Mto Jordani. 
Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.

Tendo la pili; 
Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana.  
Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.

Tendo la tatu; 
Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. 
Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.

Tendo la nne; 
Yesu anageuka sura. 
Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.

Tendo la tano; 
Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia.  
Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.

49 comments:

  1. Asanteni nlikua sina kitabu chenye rozali sasa nitasali mafungu.

    ReplyDelete
  2. Asanteni sana. Mungu awabariki

    ReplyDelete
  3. Asante sana kwa kuniwezesha kusali muda wowote

    ReplyDelete
  4. Nashukuru sana kwa haya mafungu.Mkipata Rosari ya Huruma,Machungu saba,Bibi Yetu,Mikaeli mnaeza ongezea tafadhali

    ReplyDelete
  5. Asante kwakutu injilisha mungu awabariki

    ReplyDelete
  6. Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi. Asanteni kwa huduma hii.

    ReplyDelete
  7. Asanteni sana kwa kutuinjilisha kupitia sala hizi takatifu

    ReplyDelete
  8. Nilikuwa sifahamu vizuri lakini kwa somo hili hakika kusali rozali itakuwa rahisi sana.Asanteni

    ReplyDelete
  9. Shukran sana kwa maelekezo na utaratibu wa kusali rosali pamoja na sala.
    Be blessed abundantly




    ReplyDelete
    Replies
    1. Asanteni sana Baraka za bwana zikae nanyi siku zote

      Delete
  10. Mama wa msaada utuombee sisi wanao.Tusali rozali jamani,mama huyu ni mgawa neema,anayo mamlaka makubwa aliyopewa na mwanaye bwana wetu Yesu Kristo.Tumkimbilie kwa imani naye atatufikishia maombi yetu kwa mwanaye Yesu Kristo

    ReplyDelete
  11. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  12. ๐Ÿ™nafarijika Sana kusali Rozali takakatifu๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ™

    ReplyDelete
  13. Asante saana wapendwa. Moyo wangu umejaa furaha kubwa, nikitafakari nakumuliliya muumba wetu kupitiya kwa mama wetu Bikira Maria kwakusali haya matendo ya rozari takatifu.

    ReplyDelete
  14. Mbarikiwe sana kwa uinjilishaji huu๐Ÿ™

    ReplyDelete
  15. Ahsanteni sana ila amjaweka ritania.

    ReplyDelete
  16. Ahsante kwa kunifikishia ujumbe huu muhumu

    ReplyDelete
  17. Bwana Yesu Asifiwe.
    Jina La Bwana lihimidiwe Milele yote.
    Utukufu kwa Utatu Mtakatifu.
    1. Baba Iliyetuumba
    2 Mwana Aliyetukomboa kwa Damu ya Thamani kubwa.
    3. Roho Mtakatifu Mfariji na Mtoa Vipaji. Amen.
    Naombeni kupata Nakala ya Kupakua au Downloads. Ahsanten

    ReplyDelete
  18. Mbarikiwe sana. Maana wengi tunapona kupitia hizi rozari muhimu ni kusali kwa imani

    ReplyDelete
  19. Asanteni mno let's pray until something hapen...

    ReplyDelete
  20. Asante kwa uinjilishaji huu. Mungu awape nguvu na maarifa tele.

    ReplyDelete
  21. Jamn wapendwa mbarikiwe wote
    Intsagram@paggstore

    ReplyDelete
  22. Thank you very much may God bless you abundantly

    ReplyDelete